Uchaguzi wa rais na bunge ni mtihani mkubwa kwa chama tawala cha SWAPO ambacho kimetawala katika taifa hilo lenye utajiri wa madini tangu lijipatie uhuru miaka 34 iliyopita na kinakabiliwa na uchaguzi wenye upinzani mkali.
Baadhi ya wapiga kura walikuwa kwenye foleni usiku baada ya mamlaka kuruhusu vituo vya kupigia kura kufunguliwa baada ya muda uliopangwa wa kuvifunga saa tatu usiku siku ya Jumatano kutokana na kuwa watu wengi sana walikuwa bado wakisubiri kupiga kura.
Baadhi ya vituo vya kupigia kura vilianza hata hivyo kuhesabu kura.
“Kuna vituo vya kupigia kura ambavyo vimeanza kutangaza matokeo, kuna vituo vya kupigia kura ambavyo vinatwambia viliamrishwa kusitisha zoezi la kuhesabu kura,” alisema Christine Aoachamus kutoka chama kikuu cha upinzani, Independent Patriots for Change(IPC).