Kambi kuu ya upinzani ya Labour yaitikisa Uingereza

Mpinzani amevaa kinyago cha sura ya waziri mkuu

Uingereza imeingia katika wasiwasi wa kisiasa Ijumaa baada ya chama cha Labour, kambi kubwa ya upinzani, kupata nafasi isiyo ya kawaida kurudi tena katika uchaguzi.

Kuibuka kwa chama cha Labour kumekizuia chama cha conservative kinachotawala kupata kura za wingi katika Bunge la Uingereza, kwa sehemu kubwa, na moja kwa moja shukrani za matokeo hayo zitakwenda kwa wapiga kura vijana.

Katika kile ambacho kitauweka uchaguzi huu kuwa wenye kumbukumbu zaidi katika historia ya hivi karibuni nchini Uingereza ni kule May Kubahatisha katika fikra yake ataweza kuongeza wanachama wake kuwa wengi bungeni, jambo ambalo limeshindikana vibaya sana.

Hali hiyo pia imepelekea kuwa na shaka kama ataweza kuendelea na kuongoza serikali ya uchache akisaidiwa na chama cha Unionists cha Ireland ya Kaskazini.

Kulikuwa na matamko Ijumaa kutoka chama cha Labour, viongozi wa vyama vingine na kutoka kwa baadhi ya Waconservative wakimtaka waziri mkuu kjiuzulu.

Lakini May ameweka bayana kuwa atajaribu kubakia katika nafasi yake na kutafuta njia ya kuendelea kuongoza baada ya chama cha Unionist kumpa uhakika wa kumsaidia.

Maafisa wa ofisi ya Waziri Mkuu wamesema kuwa May ataelekea Buckingham Palace ili kuomba ridhaa ya Malkia kuunda serikali.

Mpango wake ni kuendelea kuongoza kwa kushirikiana na Chama cha Unionists na hivyo kumfanya awe ana kiti kimoja cha uwingi ndani ya bunge.

Mpango wa May utakuwa baada ya hapo kukabiliana na kura ya ridhaa ya bunge la Uingereza wiki ijayo.

Pamoja na ghadhabu ya wapiga kura kutokana na uamuzi wake kuitisha kura ya maoni kwa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya na namna alivyo endesha kampeni yake, watunga sheria wa chama cha Conservative walionekana tayari kwa kipindi kifupi kukubaliana naye.

Iwapo May atashindwa kupata ridhaa ya bunge katika kura ya wiki ijayo, itawapa chama cha Labour nafasi ya kuunda serikali yake ya mseto, au itaomba kuongoza kama serikali ya wachache, ijapokuwa haijafahamika iwapo chama cha Labour kitaweza kufanikisha hilo.