Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:40

Comey kutoa ushahidi dhidi ya Trump


Rais Donald Trump- Mkurugenzi wa FBI wa zamani Jim Comey
Rais Donald Trump- Mkurugenzi wa FBI wa zamani Jim Comey

Mkurugezni wa FBI Jim Comey aliyefukuzwa kazi ataieleza Kamati ya Usalama ya Baraza la Seneti Alhamisi kuwa Rais Donald Trump alimtaka athibitisha utiifu wake kwake.

Trump alisema hayo wakati wa mazungumzo yao ikulu ya White House kufuatia uchunguzi wa FBI unaowahusu maafisa wa utawala wa ikulu wapya na wazamani ukimhusisha rais mwenyewe.

Kamati imetoa mapema nakala ya tamko lake Comey la kurasa saba siku mmoja kabla ya mahojiano naye.

Hili limekuja muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taifa na maafisa wa usalama wa ngazi ya juu wengine kukataa kujibu maswali ya kamati hiyo juu ya kadhia ya Comey na uchunguzi dhidi ya Russia.

Katika tamko lake, anaeleza kwa undani vitu venye utata na kutoa mazungumzo yake katika vipindi vitano tofauti ambavyo alifanya mazungumzo na Trump, ikiwa pamoja na kauli iliyoeleza kuwa rais alijaribu kuingilia kati uchunguzi wa FBI.

“Rais alisema, Nahitaji utiifu wako na nategemea utiifu wako,” Comey ameeleza kuhusu moja ya yale yaliojiri katika mkutano mmojawapo ikulu ya White House.

“Sikusogea, wala kusema kitu au kubadilisha sura yangu katika hali yoyote baada ya kinyamao kisicho cha kawaida kilichofuatia hapo. Tulikuwa tunaangaliana hali wote tukiwa kimya.”

XS
SM
MD
LG