Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:50

Marekani yamkamata mfanyakazi akivujisha waraka wa siri mtandaoni


 Shirika la Usalama la Taifa
Shirika la Usalama la Taifa

Idara ya Sheria ya Marekani imetangaza Jumatatu kukamatwa kwa mfanyakazi alioajiriwa kwa mkataba serikalini ambaye inasemakana alituma taarifa za siri kwenye kituo cha habari kinachotumia mtandao.

Tangazo hilo limetokea siku hiyo hiyo wakati repoti ya kukamatwa kwa uvujishaji wa siri hiyo, ikisema kuwa nyaraka za siri zilizokamatwa zinaonyesha kuwa idara ya usalama katika jeshi la Russia ilijaribu kuingia katika mfumo wa usajili wa kura wa Marekani kabla ya uchaguzi wa mwaka jana.

Waraka wa kiapo uliokabidhiwa na afisa maalum wa FBI umesema kuwa mwanamke aliyekamatwa, Reality Leigh Winner, amekiri kuwa alidukua repoti hiyo ya usalama ya siri na kuituma kwa taasisi ya habari.

Kiapo hicho pia kinaeleza kwamba shirika la jumuiya ya usalama ya Marekani wametambua katika uchunguzi wao kuwa watu sita walichapisha nyaraka hiyo, akiwemo Winner, na kuwa alikuwa na mawasiliano ya email na taasisi ya habari iliyokuwa haijatajwa jina.

Tarehe zilizokuwa katika nyaraka zote zilizotajwa kwenye kiapo na ile ilionukuliwa kutokana na kukamatwa kwa udukuzi huo zinalingana.

Serikali haikusema kutoka shirika gani Winner anadaiwa alichukua waraka huo wa siri ya juu, akisema kuwa alikuwa amepewa jukumu kufanya kazi katika ofisi ya serikali ya Marekani katika jimbo la Georgia.

XS
SM
MD
LG