Waziri wa Mambo ya Ndani, James Cleverly alitia saini mkataba mpya na Rwanda siku ya Jummane, baada ya Mahakama ya Juu ya Uingereza awali kusema mipango hiyo ilikuwa kinyume cha sheria.
Lakini wabunge kutoka pande tofauti za chama hicho wameelezea huu ni “mstari mwekundu.”
Mswaada umeandaliwa kufanyakazi kulingana na mkataba mpya ambao unaiona Uingereza ikiilipa mamlaka ya Rwanda kwa ajili ya mchakato wa kuchukua waomba hifadhil ambao wanafika nchini Uingereza.
Mkataba mpya una maana kwamba Unignereza pia itawalipa majaji wa Uingereza na Jumuiya ya Madola ili kusimamia mchakato mpya utakaowekwa wa mambo pamoja na gharama zote za ada za kisheria kutoka kwa mtu yeyote atakayepelekwa Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly amesema ana imani kubwa sana kwamba mkataba mpya na Rwanda unaohusu waomba hifadhi utazungumzia changamoto za kisheria zilizotolewa na mahakama ya juu ya Uingereza.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Kigali, Cleverly alisema kwamba Rwanda imeonyesha “heshima kubwa kwa ubinadamu na utawala wa kiutalaamu kwa wakimbizi na wahamiaji” na kuonyesha “ dhahiri na bila ya tatizo lolote nia ya dhati” kwa usalama wao.
James Cleverly, Waziri Mambo ya Ndani, Uingereza: "Rwanda hivi sasa imeonyesha heshima kubwa kwa ubinadamu na utawala wa kitaaluma kwa wakimbizi na wahamiaji. Hiki ni kitu ambacho kinaeleweka kwa Uingerezaz na jumuiya mbali mbali. Mkataba ambao ulitiwa saini leo ni kazi ya pamoja. Itanchukuwa mwenendo mzuri wa kitaaluma kwamba wewe na serikali mnaonyesha na kujiweka nao katika kufanya ambayo Uingereza inaifanya kuhakikisha kwamba tuvunja ule mpango ambao umekuwa ukitumiwa na watu waovu wanaosafirisha watu kwa magendo.”
Mpango wa Rwanda ni kiini kwa serikali ya kiconservative iliyojiwekea malengo ya kusitisha waomba hifadhi wanaowasili kwa boti ndogo ndogo kuvuka mkondo wa Uingereza.
Uingereza na Rwanda walifikia makubaliano Aprili 2022 kwa baadhi ya wahamiaji ambao wanavuka kuingia Uingereza na hivyo kupelekwa nchini Rwanda, ambako maombi yao ya uhamiaji yatashughulikiwa na kama wakifanikiwa, wataruhusiwa kuendelea kuishi huko.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Vincent Biruta amesema waomba hifadhi wanakaribishwa nchini Rwanda.
Vincent Biruta, Waziri wa Mambo ya Nje, Rwanda anaeleza: “Nataka kuwathibitishia kwamba watu watakaofika Rwanda wanakaribishwa na watapatiwa yote usalama na msaada wanaohitaji kujenga maisha yao mapya. Yale ambayo yataangazia kuimarisha ushirikiano na Uingereza na kuutekeleza huu mkataba.”
Serikali ya Uingereza inadai kwamba ku wale watakaopelekwa huko watawavunja moyo wengine wanaotaka kufanya safari hatari kuvuka bahari na kuuvunja mfumo haramu wa magenge ya wasafirishaji haramu wa binadamu.
Wakosoaji wanasema ni kinhyume cha maadili na hautafanya kazi kuwapeleka wahamiaji katika nchi iliyoko takriban umbali wa kilometa 6,400, bila ya kupewa fursa ya kuishi nchini Uingereza .
Uingereza tayari imeilipa Rwanda kiasi cha dola milioni 177 kwa mujibu wa mkataba, lakini hakuna mhamiaji ambaye ameshapelekwa huko wakati kuna changamoto za kisheria.