CHADEMA yasema Katibu Uenezi wa kitengo cha  wanawake alitekwa nyara katika mji wa Kibiti

Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani CHADEMA Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukamatwa . Picha na VOA

Watu wasiojulikana walimteka nyara, kumpiga na kumjeruhi vibaya afisa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema

Watu wasiojulikana walimteka nyara, kumpiga na kumjeruhi vibaya afisa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema kabla ya kumtupa msituni, chama chake kilisema siku ya Jumapili, mwezi mmoja baada ya kutekwa nyara na kuuawa kwa kiongozi mwingine wa chama hicho.


Kesi zinazoripotiwa huenda zikachafua taswira ya mageuzi ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akisifiwa kwa kupunguza ukandamizaji tangu kumrithi John Magufuli, aliyefariki akiwa madarakani miaka mitatu iliyopita.


Wanaharakati wa haki wanasema serikali ya Samia inawalenga wapinzani kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Lakini serikali inakanusha shutuma hizo.


Chama cha CHADEMA kimesema Katibu Uenezi wa kitengo cha Wanawake cha chama hicho Aisha Machano, alitekwa nyara katika mji wa Kibiti, Mashariki mwa nchi hiyo akiwa katika majukumu yake ya kikazi.


Waendesha bodaboda walimkuta katika hali mbaya ya kiafya na maumivu makali, chama hicho kilisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.