Cameroon yaongeza maafisa wa polisi kudhibiti mmiminiko wa maelfu ya mashabiki

Ulinzi umeimarishwa kabla ya mechi ya Gambia na Cameroon Jumamsoi katika uwanja wa mpira wa Japoma, Douala, Cameroon, Jan. 29, 2022.

Ulinzi umeimarishwa kabla ya mechi ya Gambia na Cameroon Jumamsoi katika uwanja wa mpira wa Japoma, Douala, Cameroon, Jan. 29, 2022.

Kabla ya mechi ya mchujo kati ya Cameroon na Gambia katika michuano inayoendelea ya Kombe la Soka la Mataifa ya Afrika huko Douala, mji wa kibiashara na jiji lilioko pwani Jumamosi, Cameroon inasema imepeleka maafisa wa polisi wa ziada 250 kudhibiti mmiminiko wa maelfu ya mashabiki.

Taifa la Afrika ya Kati wiki hii limeripoti mkanyagano ulioua watu wanane na kujeruhi 38 katika mechi ya AFCON iluyofanyika mji mkuu, Yaounde. Polisi wamekuwa wakifanya jitihada kudhibiti idadi kubwa ya mashabiki wanaowasili.

Wenyeji wa michuano hiyo Cameroon wanacheza mechi ya robo fainali Jumamosi dhidi ya Gambia mjini Douala.

Miongoni mwa mashabiki wa Cameroon mjini humo ni Gilbert Ekosso, mwalimu mwenye umri wa miaka 28. Ekosso anasema iwapo atakosa fursa hii, huenda hatoweza kuiona Cameroon ikicheza dhidi ya Gambia katika mechi ya AFCON maishani mwake.

Mara ya mwisho Cameroon ilikuwa wenyeji wa michuano ya AFCON ni miaka 50 iliyopita,” Ekosso alisema. “Hakuna namna naweza kukosa kuangalia mechi hii kati ya Cameroon na Gambia. Inaelekea ni fursa ya pekee katika uhai kuwaona wakicheza hapa Douala.”

Jeshi la Polisi la Cameroon na Wizara ya Michezo wanasema maelfu ya mashabiki wa soka kutoka miji na vijiji mbalimbali vya Cameroon tayari wamewasili Douala. Polisi wanasema uwanja wa Japoma wenye viti 50,000, ambako mechi hiyo itachezwa, hauwezi kuhimili idadi hiyo ya mashabiki wanaopigania kupata tiketi za kuingia uwanjani.

Narcisse Mouelle Kombi ni Waziri wa Michezo na Mafunzo ya Viungo wa Cameroon.

Kombi anasema kuna idazdi kubwa ya polisi wamepelekwa kuzuia tabia hiyo isiyo ya kistaarabu ya Wakameroon wanaotaka kulazimisha kuingia uwanjani wakati hawana tiketi wala matokeo ya vipimo vinavyoonyesha hawana maambukizi ya COVID-19.

Anasema polisi watahakikisha kuwa idadi ya watu watakaoingia uwanjani ni ile inayoruhusiwa na Shirikisho la Kandanda la Afrika (CAF).

Kombi amesema kutokana na masharti ya COVID-19, CAF imeruhusu idadi ya mashabiki 35,000 kuingia uwanjani. Amesema mashabiki ambao hawajaruhusiwa kuingia uwanjani waangalie mechi hiyo katika televisheni zao.

Michuano ya AFCON ilianza Januari 9 na itmalizika Februari 6.