Burkina Faso: Waziri wa zamani wa mambo ya nje aliyehamia upinzani atoweka

KIongozi wa upinzani Ablasse Ouedraogo huko Ouagadougou> Picha na AFP

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Burkina Faso Ablasse Ouedraogo iliyehamia upinzani hajulikani alipo kwa muda wa siku tatu, baada ya kuchukuliwa kutoka nyumbani kwake na watu ambao walisema kuwa ni polisi , chama chake kimesema siku ya Jumatano.

Mbali na kuwa waziri wa mambo ya nje Ouedraogo aliwahi kuhudumu kama naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) na kushika nyadhifa kadhaa katika Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Kwa sasa ni mkuu wa chama cha upinzani cha Le Faso Autrement na amekuwa akiukosoa utawala wa kijeshi ambao umekuwa madarakani nchini Burkina tangu mapinduzi ya kijeshi ya Septemba 2022.

Mwanzoni mwa mwezi Novemba, jeshi la Burkina lilimuandikisha Ouedraogo mwenye umri wa miaka 70 katika jeshi kwa lengo kumpeleka mstari wa mbele ili kusaidia katika “mapambano dhidi ya ugaidi” katika nchi hiyo ambayo imegubikwa na uasi wa wanajihadi.

Wakati huo, chama chake cha kiasa kililaani hatua hiyo kuwa kama ya kulipiza kisasi kwa Ouedraogo kwa kuwakosoa watawala wa nchi.

Wapinzani wapatao darzen waliandikishwa jeshini ili kushirikia katika mapambano dhidi ya wanajihadi, Human Rights Watch imesema mwezi Novemba.

Chanzo Cha habari hii ni shirika la habari la AFP