Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika jimbo la Brazil la Rio Grande do Sul imeongezeka hadi 136, kitengo cha ulinzi wa raia katika eneo hilo kilisema Jumamosi, kutoka idadi ya awali ya 126 , huku watu wengine 125 wakiwa hawajulikani walipo.
Dhoruba na mafuriko yanayokumba jimbo la kusini la nchi hiyo ya Amerika Kusini lenye wakazi milioni 10.9, yamewaacha pia karibu watu 340,000 bila ya makazi, kulingana na kitengo cha ulinzi wa raia katika eneo hilo.