Safari hiyo, ya tano ya Blinken katika eneo hilo tangu shambulio la Hamas la Oktoba 7 ndani ya Israeli, inafanyika siku chache baada ya Marekani kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi, dhidi ya walengwa wanaohusishwa na Iran, nchini Iraq na Syria, ikiwa ni ongezeko la hivi punde, la kasi ya mzozo ambao Rais Joe Biden alikuwa akitaka kuuepuka.
Ziara hiyo pia inajiri huku utawala wa Biden ukielezea kukatishwa tamaa zaidi na Israel, huku vikwazo vikiwekwa Alhamisi kwa walowezi wenye itikadi kali, ingawa Marekani imepuuzilia mbali wito wa kimataifa kwa Israeli kusitisha mashambulizi yake ya kijeshi.
Pendekezo linalojadiliwa -- lililoandaliwa wakati wa mazungumzo wiki moja iliyopita mjini Paris lililohusisha mkuu wa CIA na maafisa wa Israel, Qatar na Misri – lilikusudiwa kusitisha mapigano kwa muda wa wiki sita, za kwanza, kutoa nafasi kwa kundi la Hamas kuwaachilia huru mateka waliokamatwa tarehe 7, mwezi Oktoba, huku Israeli nayo, ikiwaachilia huru wafungwa wa asili ya Palestina, kulingana na kwa chanzo cha Hamas.
Blinken katika safari yake wiki hii atatembelea Israel pamoja na Misri na Qatar.