Blinken aelekea Saudi Arabia kwa mazungumzo juu ya masuala ya usalama na uchumi

Antony Blinken Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani kwenye mkutano wa G7

Kabla ya safari yake, Blinken alisema Jumatatu kuwa Marekani “ina maslahi ya kidhati ya usalama wa taifa katika kuhamasisha kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Israeli na Saudi Arabia.”

Tukirudi nyuma, angalau hadi utawala Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, Marekani imekua ikishughulikia kurejesha uhusiano kati ya Israeli na mataifa kadhaa ya Kiarabu, ikiwemo Misri, Bahrain, Morocco na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Blinken ameuambia mkutano wa kamati ya kutetea maslahi ya Israeli hapa Marekani, AIPAC kuwa sehemu ya ziara yake Saudi Arabia itakuwa kushughulikia kufikia suala lakuwepo na uhusiano bora kati ya Israeli na Saudi Arabia.

Antony Blinken, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani akizungumza kwenye mkutano wa AIPAC.

“Tunaamini kuwa tunaweza na bila shaka lazima tutekeleze jukumu letu kuu katika kupeleka mbele hili,” Blinken alisema. “ Hivi sasa, hatuna ndoto ya kwamba hili linaweza kufanyika haraka na kwa urahisi.”

Blinken’s schedule includes a ministerial meeting Wednesday with the Gulf Cooperation Council to discuss promoting “security, stability, de-escalation, regional integration, and economic opportunities across the Middle East,” the State Department said.

Ratiba ya Blinken inajumuisha mkutano wa Jumatano na mawaziri wa mataifa wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba kujadili kupeleka mbele suala la “usalama, utulivu, kupunguza mvutano, kuunganisha pamoja kanda hiyo, na fursa za kiuchumi kote Mashariki ya Kati,” ilisema Wizara ya Mambo ya Nje.

Siku ya Alhamisi, Blinken na waziri mwenzake wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan wataongoza mkutano wa ushirika wenye nguvu wa nchi 80 zinazopambana na kikundi cha Islamic State.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.