Kabla ya kuanza ziara yake, Blinken Jumatatu aliambia kikao cha kundi linalounga mkono Israel la AIPAC kwamba moja wapo ya majukumu yake wakati wa ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano kati ya Israel na Saudi Arabia.
Blinken Jumatano anatarajiwa kufanya mkutano na mawaziri wa taifa hilo pamoja na baraza la ushirikiano wa ghuba, ili kuzungumzia usalama, udhabiti, utangamano wa kieneo pamoja na nafasi za kuchumi zilizopo mashariki ya kati, kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara yake.
Alhamisi, Blinken na mwenzake wa Saudi Arabia Faisal bin Fathan watafanya kikao cha pamoja na waakilishi kutoka mataifa 80 yanayopambana na kundi la Islamic State.
Forum