Kremlin mapema mwezi huu ilisema iko tayari kubadilishana mfungwa mwingine na Marekani, ambaye atawezesha Gershkovich kuachiliwa huru, ikiwezekana kubadilishana na Vladimir Dunaev, raia wa Russia anayezuiliwa katika jela ya Marekani kwa mashtaka ya uhalifu wa kimtandao. Lakini Moscow ilisema mashauriano hayo lazima yafanyike kwa siri.
Biden, akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari huko Finland, aliweka wazi kuwa Marekani ina maslahi katika hili.
“Nina nia ya dhati ya mabadilishano ya wafungwa,” kiongozi huyo wa Marekani alisema. “Nina nia ya dhati juu ya kufanya yote yatakayo wezekana kwa Wamarekani kuachiliwa huru ambao wanashikiliwa kinyume cha sheria huko Russia au mahali popote pengine kwa njia hiyo, na kuwa mchakato huo unaendelea.
Gershkovich alikamatwa kwa mashtaka ya ujasusi katika mji wa Yekaterinburg wakati akiwa safarini kutekeleza majukumu ya uandishi. Mahakama moja Moscow hivi karibuni iliendeleza uamuzi wa kumweka jela hadi August 30.
Russia imesema kuwa kubadilisha huku hakukuweza kufanyika mpaka mashtaka dhidi yake yatakapo amuliwa, lakini hakuna tarehe ya kesi iliyopangwa.