Russia jana ilitangaza kwamba imemuweka kizuizini raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 31 katika mji wa mashariki wa Yekaterinburg kwa tuhuma za ujasusi.
Gershkovic anafanya kazi katika ofisi ya gazeti hilo mjini Moscow na alikuwa na kibali rasmi cha vyombo vya habari vya Russia, Wall Street Journal imesema. Amekuwa akifanya kazi nchini Russia tangu mwaka wa 2017.
Idara ya usalama ya Russia, FSB ilitoa taarifa ikisema imesitisha shughuli haramu za Gershkovich, ikisema anashukiwa kufanya ujasusi kwa maslahi ya serikali ya Marekani.
Gazeti hilo limekanusha madai hayo na kuomba Gershkovich aachiliwe huru mara moja.
Msemaji wa White House Karine Jean Pierre alisema katika taarifa kwamba wizara ya mambo ya nje ya Marekani imekuwa ikiwasiliana moja kwa moja na serikali ya Russia kuhusu kukamatwa kwa mwandishi huyo wa habari.
“Serikali ya Russia kuwalenga raia wa Marekani ni jambo lisilokubalika, “Jean Pierre amesema.