Gershkovic alikamatwa mwishoni mwa mwezi Machi wakati akisafiri kufanya kazi ya kuripoti katika mji wa Yekaterinburg.
Jaji aliamua mwezi Mei kwamba ataka rumande hadi tarehe 30 Agosti, uamuzi ambao mawakili wake wamejaribu kuupinga leo Alhamisi bila mafanikio.
Gershkovic na Wall Street Journal walikanusha kwamba mwanahabari huyo alijuhusisha na shughuli za ujasusi.
Serikali ya Marekani ilisema Gershkovic amezuiliwa kinyume cha sheria na iliomba aachiwe huru mara moja.
Tarehe ya kesi yake haikutangazwa.
Forum