Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano anatarajiwa kusaini amri kadhaa za kiutendaji katika hatua za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Msemaji wa White House Jen Psaki Jumanne aliwaambia waandishi wa Habari kwamba Biden anaamini kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni moja ya mizozo mikubwa ya kushughulikia katika muda wa utawala wake.
Biden alimteua waziri wa zamani wa mambo ya nje John Kerry kuhudumu kama mwakalishi wake wa masuala ya hali ya hewa.
Miongoni mwa hatua ambazo Biden anatarajiwa kuchukua ni kusitisha kukodisha ardhi na maeneo ya maji ya serikali kwa ajili ya shughuli za uchimbaji wa gesi na mafuta, na kuweka sheria za kupunguza viwango vya gesi chafu.