Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliapa siku ya Jumamosi kuendeleza vita vya Israel dhidi ya Hamas hadi ushindi, akiendeleza mashambulizi yake huko Gaza katika mkesha wa kumbukumbu ya siku 100 za vita.
Vita hivyo vilichochewa na shambulio la Hamas la Oktoba 7 kusini mwa Israel, siku mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo. Zaidi ya watu 1,200 wameuawa nchini Israel na karibu watu 24,000 huko Ukanda wa Gaza wameuawa zaidi ya asilimia 1 ya wakazi wa Gaza.
Wakati huo huo, maelfu ya watu walianza maandamano ya saa 24 mjini Tel Aviv Jumamosi usiku, wakiitaka serikali kuwarudisha mateka nyumbani baada ya siku 100 ambao wanashikiliwa na Hamas.
Waandamanaji, wakiwa na picha za watu waliotekwa nyara, walikusanyika katika uwanja uitwao Hostages Square mkabala na Wizara ya Ulinzi ya Israel ambayo imekuwa mahali pa kukutana kwa watu hao.