Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:28

Israel yafanya mashambulizi usiku kucha dhidi ya Gaza


Picha iliyochukuliwa kutoka Rafah ikionyesha mosha ukipaa angani kwenye mji wa Khan Younis. Jan. 13, 2024.
Picha iliyochukuliwa kutoka Rafah ikionyesha mosha ukipaa angani kwenye mji wa Khan Younis. Jan. 13, 2024.

Vikosi vya Isreal vimeishambulia Gaza Ijumaa usiku kucha hadi Jumamosi asubuhi, wakati vita dhidi ya  wanamgambo wa Hamas vikikaribia siku 100.

Shirika la habari la AFP limewanukuu baadhi ya mashuhuda wakisema kwamba makombora ya Israel Ijumaa yalipiga miji ya kusini mwa Gaza ya Khan Younis na Rafah. Kampuni kuu inayosambaza huduma za internet huko Gaza imesema kwamba mawasiliano yote yalikatwa Ijumaa, ikiwa ni matokeo ya mashambulizi ya Israel.

Jeshi la Israel limesema kwamba vikosi vyake vimewaua wanamgambo watatu walioshambulia makazi ya walowezi wa Kiyahudi huko Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu. Taarifa ya jeshi imesema kwamba wanamgambo waliingia kwenye makazi ya walowezi ya Adora, takriban kilomita 20 magharibi mwa mji wa Hebron. Jeshi limesema wanajeshi wake walishambuliwa walipofanya msako katika eneo hilo.

Andrea De Domenico, mkuu wa ofisi ya UN kwa uratibu wa masuala ya kibinadamu katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu, amesema Ijumaa kwamba Israel imekuwa na, “utaratibu maalum wa kutuzuia kuzisaidia hospitali, jambo ambalo linafikia kiwango cha unyama, ambacho kwangu mimi, hata huwezi kukifikiria.”Amesema.

Forum

XS
SM
MD
LG