Balozi wa Ubelgiji aishauri DRC kufungua mashitaka dhidi ya Rwanda

Moja wa mitaa Kinshasa, mji kuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Picha na REUTERS/Thomas Mukoya

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni vyena  iwasilishe malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki juu ya Rwanda kushindwa kuheshimu mipaka yake, balozi ya Ubelgiji  nchini Congo amesema  siku ya Ijumaa katika mkutano wa kutathimini kwa undani mgogoro wa Mashariki mwa Congo.

Congo imekuwa ikijitahidi kuwarudisha nyuma waasi wa M23 tangu walipoanza upya mashambulizi katika eneo la Mashariki ambalo tayari lilikuwa na ghasia mwaka 2022.

Mapigano hayo yamesababisha watu zaidi ya 738,000 kupoteza makazi katika miezi ya mwanzo ya mwaka huu peke yake, kulingana na shirika la Misaada la Umoja wa Mataifa OCHA.

Serikali ya Congo, Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi ikiwemo Marekani, Ubelgiji wamekuwa wakiishutumu Rwanda kwa kuliunga mkono kundi la M23- ikiwa ni pamoja na kuwapatia silaha na wanajeshi- kitu ambacho Rwanda imekuwa ikikikanusha mara kwa mara.

Katika mkutano wa wawakilishi wa nchi za nje huko katika mji wa mashariki wa Goma, balozi wa Ubelgiji nchini Congo, Roxane de Bilderling amesema mengi lazima yafanywe kuiwajibisha Rwanda.