Bahari ya Hindi: Ripoti ya awali yaeleza Hakuna aliyenusurika katika ajali ya meli

Eneo pana la Australia lenye operesheni za uokoaji, kilomita 5,000 kuelekea magharibi mwa Perth, mji mkuu wa taifa hilo la Australia Magharibi.

Hakuna mtu yeyote aliyenusurika baada ya meli ya uvuvi iliyokuwa imebeba mabaharia 39 raia wa China, Indonesia na Ufilipino kuzama wiki iliyopita katika Bahari ya Hindi, kulingana na ripoti ya uchunguzi wa awali ya serikali iliyotolewa Jumanne.

Meli hiyo ya China ilipinduka Mei 16, ikiwa na Wachina 17, Waindonesia 17 na Wafilipino watano.

“Katika uchambuzi wa kuzama kwa meli hiyo … matokeo ya awali yanasema hakuna aliyenusurika kwenye meli hiyo,” wizara ya uchukuzi wa Beijing alisema katika taarifa aliyoiweka katika mtandao rasmi wa kijamii.

Boti hiyo ilizama katika eneo pana la Australia lenye operesheni za uokoaji, kilomita 5,000 kuelekea magharibi mwa Perth, mji mkuu wa taifa hilo la Australia Magharibi.

Vyombo vya habari vya serikali ya China viliripoti Jumatatu kuwa miili saba ilipatikana katika operesheni ya uokoaji iliyofanywa na boti za China na Sri Lanka, bila ya kuainisha mataifa ya waliofariki katika ajali hiyo.

Australia ilituma ndege tatu na meli nne kusaidia katika juhudi hiyo ya kimataifa ya kutafuta na uokoaji.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP