Kwa zaidi ya muongo mmoja, mataifa hayo ya Afrika kwa ujumla yametajwa na taasisi ya Transparency International katika ripoti yake ya mwaka kuwa hayajafanya vizuri. Ripoti hiyo imetolewa Jumatano.
Eneo la kusini mwa jangwa la Sahara linaendelea kufanya vibaya kulingana na orodha ya kila mwaka ya Transparency International, huku Somalia ikiwa katika nafasi ya chini kati ya mataifa 180 kwa mwaka wa 12 mfululizo.
Orodha hiyo imebaini kuwa zaidi ya theluthi mbili ya nchi ambazo zimefanyiwa utafiti zina alama ya chini ya 50 kwenye kiwango cha 100, huku wastani wa kawaida ukiwa ni 43. Mataifa ya Afrika yalipata alama 32. Somalia ikiwa imepata alama tisa tu.
Mshauri wa eneo la kusini mwa Afrika kwa Transparency International, Kate Muwoki, amelizungumzia bara la Afrika kwa mwaka uliopita kuwa, “serikali nyingi za kiafrika zimeshindwa kuzungumzia rushwa katika eneo hilo, ingawaje tuna viongozi ambao wamewekwa katika mifumo ya majibu ili kujenga taasisi zenye nguvu na kubadili mwenendo wa kitabia.
Kwa hiyo waati ambapo kuna dalili za matumaini, nchi zilizo juu katika orodha hiyo ni Bostwana, Seychelles, Cabo Verde, Rwanda na Namibia, ambao walipata alama zaidi ya 50.
Katika nchi ambazo ziko chini kwenye orodha hiyo, na hazijonyesha mabadiliko makubwa. Ziko nchi kama Sudan Kusini, Somalia ambayo iko chini kabisa, nan chi ambazo zimeshuke ni Malawi, Madagascar, Msumbiji na Guinea Bissau.”
Lakini anasema Umoja wa Afrika na viongozi kadhaa wakuu, hasa marais wa mataifa mawili yenye uchumi mkubwa katika bara hilo Nigeria na Afrika Kusini hivi karibuni wamefanya suala la utawala safi ndiyo kiini.
Mwaka 2017 pia tumeona kuangula kwa viongozi kadhaa ambao walishutumiwa kwa makubaliano yenye kutia mashaka – Yahya Jammeh wa Gambia, Jose Eduardo Dos Santos wa Angola, Robert Mugabe wa Zimbabwe na hivi karibuni, Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Kadhia ya ngazi ya juu ya rushwa pia imetia doa kwa waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, ambaye alijiuzulu mapema mwezi Februari kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali.
Mrithi wa Zuma, Cyril Ramaphosa, amefanya mapambano ya rushwa ndiyo suala lake kuu. Mfanyabiashara huyo bilionea wiki hii amewataka maafisa wa juu wa serikali kufanyiwa ukaguzi, kuanzia yeye mwenyewe.
“Hivi sasa, kama kuna kitu chochote ambacho wananchi wengi wa Afrika Kusini wangependa kukiona, ni mwenendo wa kufanyiwa ukaguzi wawakilishi wao wa umma. Hivi sasa ni kitu ambacho naanimi kinaweza kufanyika, na hili litafanyika kuanzia na mtendaji mkuu katika nchi, ndiyo hili litafanyika hivyo,” amesema Ramaphosa.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari hivi karibuni alitangaza kuwa mali zote za taifa zitafutwe, alisema hayo katika harakati za karibuni dhidi ya rushwa na kusema mali zitakazopatikana zitauzwa kwa manufaa ya hazina. Buhari pia ni mwenyekiti wa kwanza wa AU ambaye ameweka suala la kupambana na rushwa ni kipaumbele.
Muwoki anasema kwamba taasisi hiyo ya ulimwenguni imeelezea maendeleo haya na kuongeza kuwa mwaka 2018 utakuwa ni muhimu sana barani humo. Tumeona nia ya dhati kutoka Umoja wa Afrika na kutoka kwa viongozi katika kikao cha karibuni kilichofanyika Addis Ababa. Inatia moyo sana na kwa hakika hili tunaliunga mkono.”
Anasema njia bora huenda ikawa ni kuondoa wingu jeusi la rushwa, kwa kuleta mwanga wenye kung’ara.