Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:50

Lungu ataka Afrika ishirikiane kutokomeza ukoloni mamboleo


Rais Edgar Lungu
Rais Edgar Lungu

Rais wa Zambia Edgar Lungu amesema kwamba nchi za kiafrika zinatakiwa kushirikiana ikiwa ni msingi wa kujikwamua dhidi ya ushawishi wa ukoloni wa mataifa ya kigeni.

Rais Lungu ambaye yuko nchini Rwanda kwa ziara ya siku mbili baada ya kutembelea jumba la makumbusho ya mauaji ya halaiki yaliotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Rais Edgar Lungu amefuatana na mawaziri wake wa mashauri ya kigeni, ulinzi na usalama pamoja na viongozi wengine waandamizi katika serikali ya Zambia.

Rais Lungu pamoja na maeneo mbalimbali aliyotembelea ikiwa ni pamoja na eneo maalum la viwanda vya kisasa pembezoni mwa jiji la Kigali, ametembelea pia jumba la makumusho ya mauaji ya halaiki ambao masalia ya miili ya zaidi ya watu lakini mbili na nusu imehifadhiwa.

Rais Lungu amesema: "Watu wote waliohusika kwenye mauaji ya kimbari popote wanafahamika nadhani kinachofuatia sasa ni kutazama makubaliano ya kisheria yaliyoko baina ya Rwanda na Zambia na kuangalia uwezekano wa kuharakisha utekelezwaji wa makubaliano hayo.

Zambia haitakiwi kuwahifadhi watu hao na wala haitakubali kuwahifadhi wavunjaji wa sheria ni lazima watu hawa wakamakatwe na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria kujibu unyama walioutenda, amesema."

Rais Edgar Lungu amesema matatizo ya nchi za kiafrika kwa kiasi kikubwa yamekuwa na uhusiano wa mabaki ya ushawishi wa nchi za kigeni ambazo zilileta ukoloni kwa waafrika akasema mpaka sasa nchi hizo bado zinaonyesha ushawishi na kuwagawa waafrika kwa misingi ya ukabila, huku akitoa mfano wa nchi yake Zambia.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Sylivanus Karemera, Rwanda

XS
SM
MD
LG