Mapinduzi ya mwezi uliopita yamezusha wasi wasi miongoni mwa washirika wa Magharibi na nchi za kidemokrasia za Afrika ambazo zinahofia kwamba hatua hiyo inaweza kuyaruhusu makundi ya Kiislamu yenye harakati zake katika eneo la Sahel na kupanua uwepo wao na kuipa Russia nafasi ya kuongeza ushawishi wake.
Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi- ECOWAS imekuwa ikijaribu kufanya mashauriano na utawala wa kijeshi lakini imesema iko tayari kutuma wanajeshi Niger kurejesha utaratibu wa kikatiba kama juhudi za kidiplomasia zitashindikana.
Baraza la amani na usalama la AU limesema katika taarifa yake Jumanne kwamba inazingatia uamuzi wa kuliweka tayari jeshi la ECOWAS na kuiomba tume ya AU kutathmini matokeo ya kiuchumi , kijamii na kiusalama ya kupeleka jeshi kama hilo.
Maazimio katika taarifa ya Jumanne yalipitishwa kwenye mkutano wa baraza uliofanyika Agosti 14 .
Ecowas inataka kuachiliwa haraka rais Mohamed Bazoum aliyekamatwa tangu wakati wa mapinduzi .
Chanzo cha habari hii ni mashirika mbalimbali ya habari