Majambazi hao wakiwa na silaha za moto walifanikiwa kupora silaha saba kutoka kwa askari hao katika maeneo ya Mkenge Wilayani Kibiti Mkoani Pwani.
Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema kuwa inalaani kitendo hicho na kuahidi kuwashughulikia wote waliohusika na mauaji hayo.
Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Nsato Marijani Msanzya amesema kuwa askari hao 8 wameuawa wakiwa njiani kuelekea kambini wakitokea lindoni eneo la Jaribu Mpakani mara baada ya kuwekewa mtego na wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Aidha Kamishna huyo amekataa kulihusisha tukio hilo na ugaidi huku akisema hakuna haja ya kuanzisha kanda maalum ya kipolisi katika mkoa wa Pwani licha ya kutokea mashambulio ya kuwaua maafisa wa jeshi la polisi mara kwa mara katika eneo hilo.
“Hili sio tukio la mara ya kwanza kwa mauaji ya aina hiyo yanayowalenga askari polisi kutokea katika maeneo ya wilaya ya mkuranga mkoani pwani wakiwemo viongozi wa serikai na watendaji mbalimbali hali inayozidisha hofu kwa wananchi wa maeneo hayo kuhusiana na usalama wao na mali zao,” ameeleza Kamanda Msanzya.
Ameongeza kuwa uonevu huo unaofanywa dhidi ya askari wa jeshi hilo sasa umefika mwisho na kusema kuwa jeshi hilo linaingia kwenye opresheni maalum ya kuwasaka wahalifu hao kwa lengo la kukomesha vitendo vya kikatili vya mauaji vinavyofanywa na makundi ya wahalifu dhidi ya polisis na hata raia.
Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.
Polisi pia imesema kuwa baada ya majambazi hao kufanya mauaji kwa askari walifanikiwa kuchukua silaha tisa kati ya hizo SMG nne zikiwa na risasi 30 na silaha aina ya long range tatu na risasi zake.
Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa awali gari ya polisi ilikuwa ikitokea eneo la Jaribu mpakani kwenye kizuizi cha barabara kuelekea Bungu, baada ya kubadilishana shift nyingine ndipo walipofika maeneo ya Mkengeni sehemu yenye mteremko na majani marefu.
Hapo walianza kushambuliwa na najambazi kwa kupigwa risasi. Risasi zilipigwa kioo cha mbele usawa wa dereva na kusababisha dereva kupoteza muelekeo na gari kuingia kwenye mtalo wa barabara na ndipo majambazi hao kufanya mauaji kwa askari.