Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 07:39

Uzbekistan: Sweden ilionywa juu ya mshukiwa wa shambulizi la lori


Watu wanaendelea na maisha ya kawaida huko Stockholm baada ya shambulizi la lori katika duka kubwa liliowalenga kundi la watu.
Watu wanaendelea na maisha ya kawaida huko Stockholm baada ya shambulizi la lori katika duka kubwa liliowalenga kundi la watu.

Vyombo vya usalama vya Uzbekistan vilitoa habari kuhusu Rakhmat Akilov, mtu ambaye anatuhumiwa kwa kuelekeza lori lililokuwa katika mwendo kasi kwenye kundi la watu.

Tukio hilo lilitokea huko Stockholm wiki iliopita, upande wa Magharibi kabla ya shambulizi hilo la mauaji, Waziri wa Mambo ya Nje Abdulaziz Kamilov amesema Ijumaa.

Kamilov amewaambia waandishi Akilov alikuwa ameiingizwa katika kundi la wapiganaji wa Islamic State baada ya kuondoka katika nchi hiyo ya Asia ya Kati mwaka 2014 na kuhamia Sweden.

“Kwa mujibu wa taarifa tulizokuwa nazo, aliwahimiza kwa hamasa kubwa raia wenzake kusafiri kwenda Syria ili waweze kupigana na upande wa Islamic State,” Kamilov amesema, akiongeza kuwa Akilov alitumia pia ujumbe wa mitandao kuhamasisha watu hao.

“Mapema (kabla ya shambulizi hilo), taarifa za Akilov za uvunjifu wa amani zilikuwa zimefikishwa na vyombo vya usalama kwa mmoja ya washirika wetu wa nchi za Magharibi ili Sweden ipewe taarifa juu ya mtu huyu,” alisema bila ya kuitaja nchi iliyotoa habari hizo au taasisi.

Chanzo cha vyombo vya usalama Uzbek kimesema wiki hiii kwamba Akilov alijaribu kusafiri kwenda Syria yeye mwenyewe mwaka 2015 ili kujiunga na kikundi cha Islamic State lakini alikamatwa katika mpaka wa Uturuki na Syria na kurejeshwa Sweden.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa kipindi cha Februari vyombo vya usalama vya Uzbekistan vilimuorodhesha Akilov katika jumla ya watu wanaotafutwa wakishutumiwa kwa msimamo mikali ya kidini.

XS
SM
MD
LG