Amri hiyo inapiga marufuku shughuli zote za umaa, isipokua huduma za dharura hadi Jumapili, baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais ulokua unasubiriwa kwa muda mrefu.
Msemaji wa polisi Abdifatah Adan Hassan, amewaambia waandishi wa habari kwamba, masharti yataanza kutumika kuanzia saa tatu usiku siku ya Jumamosi tarehe 14, kwa kupiga marufuku usafiri wa magari, pikipiki na watu kutembea. Masharti hayo anasema yataondolewa Jumatatu asubuhi baada ya kufanyika kwa uchaguzi.
Kuna wagombea 39 wanaopigania kiti cha rais katika taifa hilo la Pembe mwa Afrika linalopambana na uwasi unaofanywa na wanamgambo wa kislamu pamoja na kitisho cha njaa.
Uchaguzi huo unaofanyika bungeni unatarajiwa kufikisha kikomo mvutano wakisiasa ulozuka tangu kumalizika kwa mhula wa rais Mohamed Abdullahi Mohamed, maafruf kwa jina la Farmajo, bila ya kuitishwa uchaguzi mpya.
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini humo ATMIS, watahakikisha usalama nje ya eneo ambalo uchaguzi huo utafanyika, ndani ya jengo la uwanja wa ndege lenya usalama mkali.
Somalia haijaanda uchaguzi mkuu wa moja kwa moja wa kuwashirikisha wananchi kwa miaka 50 hivi sasa. Badala yake uchaguzi hufanyika kwa njia ya mchanganyiko ambapo wabunge wa serikali za majimbo pamoja na wakuu wa ukoo kuwachagua wabunge la taifa na wao ndio wanamchagua rais.