Rais Mohamed Abdullahi Mohamed ni miongoni mwa wagombea 39 wanaowania wadhifa huo wa juu nchini humo ambapo watachaguliwa na wabunge katika eneo la uwanja wa ndege.
Mshindi atarithi orodha nzito ya changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40, mzozo mkali unaoingia muongo wake wa nne, mizozo ya koo, na mapanbano ya madaraka kati ya serikali na majimbo ya serikali kuu.
"Mimi ndiye mtu anayestahili, ambaye ninaweza kuipeleka Somalia kwenye uwezo wa mtu mmoja, kura moja," Rais Mohamed, anayejulikana kama Farmaajo kwa kupenda sana jibini za Italia, aliwaambia wabunge siku ya Alhamisi.