Serikali ya Somalia imeeleza kuwa wanajeshi wake 7 wameuwawa Alhamisi katika mji mdogo wa Wanalaweyn, kusini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu, katika shambulizi la bomu.
Kundi la al-Shabaab limesema kuwa lilihusika na mashambulizi hayo mawili, yaliyotokea siku ya Jumatano na Alhamisi.
Naibu Gavana wa Jimbo la Shabelle Ali Nur ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanajeshi hao waliuwawa pamoja na kamanda wao wakati bomu lilipolipua gari waliokuwa wakisafiria wanajeshi hao.
Shambulio hilo ni la pili kufanyika katika muda wa siku mbili baada ya shambulio jengine kutokea Jumatano katika mji huo wa wanalaweyn na kuwaua watu 14.