Ajali ya meli yahofiwa kuuwa mamia Zanzibar

Rais Dk. Ali Mohamed Shein akiongoza zoezi la uokoaji Nungwe baada ya ajali ya meli Jumamosi asubuhi

Meli hiyo ya abiria ilikuwa inatoka Unguja kuelekea Pemba ikiwa na abiria 610 ndani yake

Mamia ya watu inahofiwa wamefariki dunia kufuatia kuzama kwa meli ya abiria - LCT Spice Islanders - katika bahari ya Hindi ikiwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba. Ajali hiyo imetokea katika pwani ya Nungwi, mkoa za Kaskazini Unguja.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Maelezo Zanzibar imemkariri naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi, akisema ajali hiyo ilitokea Ijumaa huku meli hiyo ikiwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.

Maafisa wa serikali wanasema mpaka Jumamosi asubuhi abiria wapatao 250 walikuwa tayari wameokolewa kufuatia juhudi za maboti binafsi yendayo kasi na jeshi polisi. Waliookolewa wamerejeshwa Unguja kuungana na ndugu zao.

Taarifa ya serikali inasema meli hiyo iliondoka katika bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ilipata hitilafu ambayo bado haijaelezewa vizuri na hatimaye kuzama.

Ajali ya meli Zanzibar

Mamia ya watu inahofiwa wamefariki dunia kufuatia kuzama kwa meli ya abiria - LCT Spice Islanders - katika bahari ya Hindi ikiwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba.