Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:14

Idadi ya vifo yaongezeka Zanzibar


Mtu aliyeokolewa katika ajali ya meli akipelekwa hospitali huko Nungwi, Zanzibar Septemba 10, 2011.
Mtu aliyeokolewa katika ajali ya meli akipelekwa hospitali huko Nungwi, Zanzibar Septemba 10, 2011.

Maafisa wanasema inawezekana kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba watu wapatao 750

Maafisa wa Tanzania wanasema idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya meli ya abiria katika mwambao wa Zanzibar Ijumaa usiku sasa inafikia watu 197.

Ripoti kutoka Zanzibar zinasema meli hiyo ya abiria, MV Spice Islander, inawezekana kuwa ilikuwa imebeba watu wengi zaidi kuliko ilivyoripotiwa awali, ikiwa na watu wapatao 750 pamoja na mizigo.

Ripoti mpya za vifo kutoka Zanzibar zinasema kuna watu 579 ambao wanajulikana kuwa walinusirika katika ajali hiyo, ingawa wengine wamejeruhiwa vibaya.

Makundi makubwa ya watu walikusanyika mahali ambapo miili ya maiti ilichukuliwa kuhesabiwa, wakitumai kupata habari za ndugu na jamaa zao ambao walikuwa katika meli hiyo.

Meli hiyo ilizama Ijumaa usiku wakati ikisafiri kutoka Unguja kwenda Pemba. Hakuna habari kamili hadi sasa kuhusu idadi kamili ya watu waliokuwa ndani ya meli hiyo au hali ya meli yenyewe wakati ilipoanza safari.

Viongozi wakuu wa serikali Zanzibar na Tanzania wamekuwa wakitembelea wagonjwa na kufariji waliofiwa katika ajali hiyo.

Ajali ya meli Zanzibar

XS
SM
MD
LG