Afrika Kusini na Angola kuongeza ushirikiano wa biashara na uwekezaji

Rais wa Angola, João Lourenço akiwa na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amempokea  rais mwenzake wa  Angola mjini Pretoria , Afrika kusini , Joao Lourenco  kabla ya Mkutano wa biashara wenye lengo la kuongeza ushirikiano wa biashara na uwekezaji baina ya pande mbili.

Mkutano huo wa biashara wa Afrika kusini na Angola umeandaliwa na wizara ya biashara , viwanda na ushindani.

Kikao hicho kati ya Ramaphosa na Lourenco kinatarajiwa kuwakutanisha Pamoja washiriki kutoka taasisi za maendeleo ya fedha, viongozi wa biashara na maafisa wa juu wa serikali.

Mkutano huo utajadili njia za kuinua biashara na uwekezaji wa kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili ya kusini mwa Afrika.

Pia utajadili kuhusu ushirikiano wa sekta muhimu za kilimo , nishati, huduma za afya, madini, mafuta na gesi.

Sekta ya uchimbaji madini katika machimbo ya Doomkop Gold Mine magharibi ya Johannesburg Oktoba 3, 2023.