Afrika Kusini: Matokeo ya awali yaonyesha ANC kikiwa na 42% ya kura

Rais na kiongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia bungeni Mai 1, 2024. Picha na RODGER BOSCH / AFP.

Matokeo ya  awali  katika uchaguzi wa kitaifa wa Afrika Kusini yanakiweka  chama cha African National Congress (ANC) kilichotawala kwa muda mrefu kwenye asilimia 42 ya kura.

Hali hiyo inaongeza kiongeza uwezekano kwamba chama hicho kinaweza kupoteza wingi wake kwa mara ya kwanza tangu kilipopata madaraka wakati wa utawala Nelson Mandela mwishoni mwa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

Ikiwa ni asilimia 16 tu ya kura zilizohesabiwa na kutangazwa, hii ni picha ya tu baada ya uchaguzi wa Jumatano. Matokeo ya mwisho ya kura ambayo yanaweza kuleta mabadiliko makubwa zaidi katika demokrasia changa ya Afrika Kusini yalitarajiwa kuchukua siku kadhaa, huku tume huru ya uchaguzi ikisema yatatangazwa ifikapo Jumapili.

Waafrika Kusini wanasubiri kwa hamu kubwa kuona kama nchi yao, yenye uchumi wa juu zaidi barani Afrika, inakaribia kuona mabadiliko makubwa.

Tume ya uchaguzi ilikuwa inakadiria kuwa asilimia 70 ya wapiga kura wangepiga kura katika uchaguzi huu, kutoka asilimia 66 katika uchaguzi wa mwisho wa kitaifa mwaka 2019 ambapo ANC ilishinda kwa asilimia 57.5 ya kura katika uchaguzi huo , licha ya utendaji wake mbaya zaidi , kwa mujibu wa wapiga kura.

Uchaguzi huu ulionekana kama kura ya maoni ya moja kwa moja juu ya utawala wa miaka thelathini wa ANC, ambao ulitoa uhuru kwa Afrika Kusini kutoka katika utawala wa kibaguzi na ukandamizaji wa apartheid katika uchaguzi wa kihistoria wa mwaka 1994 lakini umepungua umaarufu wake kwa miaka 20 iliyopita.

Mwaka huu unaweza kuwa ni wakati ambapo Waafrika Kusini wengi wanageuka kutoka ANC na kuinyima wingi wake kwa mara ya kwanza.

Matokeo yaliyotangazwa ni kutoka vituo vya kupigia kura 4,000 kati ya zaidi ya 23,000 katika majimbo tisa Afrika Kusini ambapo mchakato wa kuhesabu kura unaendelea. Karibu watu milioni 28 kati ya wakazi milioni 62 wa Afrika Kusini walisajiliwa kupiga kura.

Swali kubwa katika uchaguzi huu ni je, huu ni mwisho wa utawala wa ANC katika demokrasia, baada ya utawala wa apartheid Afrika Kusini ? Kura kadhaa za maoni zilikuwa imeonyesha kuwa ANC ikuwa chini ya asilimia 50 kabla ya uchaguzi, hali isiyokuwa ya kawaida.

Rais wa Afrika Kusini na kiongozi wa ANC Cyril Ramaphosa alisema baada ya kupiga kura Jumatano kwamba bado anaamini chama chake kitapata “wingi wa kutosha,” lakini kinakabiliwa na upinzani zaidi kuliko hapo awali.

Upinzani wa kisiasa umegawanyika kati ya vyama kadhaa, hata hivyo, na ANC bado inatarajiwa kuwa na viti vingi zaidi bungeni. Lakini ikiwa kura yake itashuka chini ya asilimia 50 kwa mara ya kwanza, itahitaji muungano ili kubaki madarakani na makubaliano na wengine kumchagua tena Ramaphosa. Hilo halijawahi kutokea kabla.

Waafrika Kusini wanapiga kura kwa vyama na si moja kwa moja kukchagua rais wao katika uchaguzi wa kitaifa. Vyama hivyo hupata viti bungeni kulingana na sehemu yao ya kura na wabunge humchagua rais. ANC imekuwa na wingi wa bunge wazi tangu mwaka 1994 na hivyo rais amekuwa akitoka ANC.

Ingawa kura nyingi bado hazijahesabiwa, matokeo ya awali yameweka chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance kwenye asilimia 25 na chama cha Economic Freedom Fighters kwenye asilimia 8. Pia imeonyesha upinzani wa haraka wa chama kipya cha MK cha Rais wa zamani Jacob Zuma, ambaye amehama ANC ambako alikuwa kiongozi wa juu. Katika matokeo ya awali Chama cha MK kilikuwa nyuma tu ya EFF.

Utabiri wa tume ya uchaguzi umebaini ushiriki mkubwa wa wapiga kura Jumatano, huku Waafrika Kusini wakiwa wamejipanga foleni hadi usiku katika mistari mirefu ya wapiga kura ikifufua kumbukumbu kwa baadhi ya uchaguzi wa kihistoria wa 1994 ambao ulibadilisha nchi.

Ingawa vituo vya kupigia kura vilifungwa rasmi saa 3 usiku, upigaji kura uliendelea kwa masaa mengi baada ya hapo katika sehemu nyingi kwani maafisa waliona ongezeko la kura za mwisho katika miji mikuu kama Johannesburg na Cape Town. Sheria zinasema kwamba mtu yeyote aliye kwenye foleni kwenye kituo cha kupigia kura kufikia wakati wa kufungwa lazima aruhusiwe kupiga kura.

Ilipendekeza kuwa Waafrika Kusini walijitokeza katika uchaguzi huu kufuatia umuhimu

Afrika Kusini ni nchi iliyostawi zaidi barani Afrika lakini imekuwa ukikabiliwa na tatizo la usawa wa rasilimali ambapo mamilioni ya wananchi badi wako katika umaskini ikiwa ni miongo mitatu baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi. umaskini uliokithiri unaathiri zaidi idadi kubwa ya Weusi ambao ni zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa nchi hiyo. Afrika Kusini ina moja ya viwango vya juu zaidi vya ukosefu wa ajira duniani na pia inakabiliwa na kiwango cha juu cha uhalifu .

Wapiga kura walibainisha masuala hayo na mengine, kama vile kashfa za ufisadi kutoka chama cha ANC kwa miaka mingi na matatizo na huduma za kimsingi za serikali, kama malalamiko yao makuu.

-Imetayarishwa na Patrick Newman, VOA, Washington, D.C.