Africa CDC : Maambukizi ya COVID-19 Afrika yafikia milioni 8.1

CDC Africa

Idadi ya maambukizi ya COVID-19 yaliyothibitishwa Afrika imefikia milioni 8.1 hadi kufikia Jumamosi mchana, Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) kimeeleza.

Kituo cha Africa CDC, shirika lililojikita katika huduma za afya cha Umoja wa Afrika, katika rekodi zake za COVID-19 lilionyesha kuwa vifo kutokana na janga hili barani kote vimefikia 206,202.

Takriban wagonjwa 7,454,718 kote barani Afrika wamepona kutokana na ugonjwa huo hadi sasa, imeelezwa.

Afrika Kusini, Morocco, Tunisia na Ethiopia ni kati ya nchi zilizokuwa na maambukizi mengi zaidi katika bara la Afrika, kwa mujibu wa shirika hilo.

Kwa kiwango cha wagonjwa, Afrika Kusini ni eneo lililoathirika zaidi, likifuatiwa na maeneo ya kaskazini na mashariki ya bara hilo, wakati Afrika ya Kati ikiwa imeathirika kidogo sana katika bara la Afrika, kwa mujibu wa Africa CDC.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African, Kenya