“Nimeshuhudia mfumo wa afya ukianguka mbele ya macho yangu,” amesema Sean Casey, ambaye ni afisa wa dharura wa WHO, wakati akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Casey alitembelea Ukanda wa Gaza kwa wiki 5 kuanzia mapema Desemba, wakati akikutana na maafisa wa afya, pamoja na wagonjwa kote kwenye eneo hilo. Casey amesema kwamba la muhimu zaidi wakati huu ni sitisho la mapigano, ingawa ufikiaji, uwezo wa watu kusafiri, pamoja na upelekaji wa misaada ya kutosha, kwa haraka, ndivyo vipaumbele vya sasa, ili kupunguza mateso wanayopitia wakazi.
Kabla ya shambulizi la Hamas la Oktoba 7, ndani ya Israel, Ukanda wa Gaza ulikuwa na mfumo dhabiti wa afya, wakati kukiwa na hospitali 36, na madaktari 25,000 wakiwemo wauguzi, pamoja na wataalam wengine.