Ufaransa imesema dawa hizo ni kwa ajili ya mateka 45 ambao wana magonjwa sugu, na kwamba utoaji huo utafanywa kwa msaada wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.
Qatar imesema makubaliano hayo pia yanajumuisha dawa na misaada mingine ya kibinadamu kwa raia wa Palestina huko Ukanda wa Gaza.
Wanamgambo wa Hamas waliwateka takriban watu 240 wakati wa shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israeli ambapo pia waliwauwa takriban watu 1,200, kwa mujibu wa takwimu za Israeli.
Baada ya hapo Israel ilianza kampeni yake ya kijeshi kuwaangamiza Hamas kutokana shambulio hilo.
Zaidi ya mateka 100 wameachiliwa baada ya mkubaliano ya muda mwezi Novemba, lakini takriban 130 wanaaminika bado wanashikiliwa na Hamas huko Gaza.
Forum