Vikwazo hivyo vimetangazwa wiki moja baada Marekani kumwekea pia vikwazo kamanda wa kikosi cha dharura RSF Mohamed Hamdan Dagalo.
Akitembelea Wad Madani, al-Burhan alikanusha tuhuma hizo akisema jeshi linapambana na adui wake ambao ni wapiganaji wa kundi la RSF.
Na mkuu wa kamisheni ya haki za binadam ya Umoja nwa Mataifa Volker Turk ameandika kwenye ukurasa wake wa X kwamba vita nchini Sudan vinageuyka na kuwa hatari zaidi kwa raia kufuatia ripoti za makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba wanamgambo wanaounga mkono jeshi la taifa wanafanya mashambulio kulenga makabila ya wachache katika jimbo la Al-Jazira.
Nae Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza na waandishi Habari Alhamisi alisema kwamba anasiukitishwa sana kwa kushindwa kumaliza vita vya Sudan na anamatumaini kwamba utawala war ais mteule Donald Trump utajaribu.
Antony Blinken, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani
"Kwangu mimi ni usikitifu wa kweli inapohusiana na Sudan, hatujaweza wakati wa utawala weyu kufikia siku ya mafanikio. Kama nilivyosema kumekuwepo na maendeleo kidogo katika kuwasilisha huduma za dharura kupitia juhudi zetu za kidiplomasia, lakini sio katika kumaliza vita, wale kukomesha unyanasaji m, walka kumaliza maafa yanayowapata wananchi. Tutaendelea kufanya kazi na nina matumaini utawala ujao utaendelea na kazi hizo."