Maandamano na mapigano baada ya wanamgambo wa Hamas kushambulia Israel

Maandamano ya kuunga mkono Israel yafanyika Manhattan, New York siku ya Jumapili, siku ya pili baada ya kundi la wanamgambo la Hamas kishambulia Israel.

Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yafanyika kwenye uwanja wa Times Square, huko Manhattan jijini New York siku ya Jumapili.

Mfululizo wa mashambulizi ya roketi yanayofanywa na wanamgambo wa kipalestina kutoka Gaza, huku makombora kutoka mfumo wa ulinzi wa Israel wa Iron Dome ukijaribu kuzuia roketi hizo kufika miji ya Israel. Oktoba 8, 2023.

Kifaru cha jeshi la Israel kinapiga doria karibu na mji wa Sderot baada ya wanamgambo wa Hamas kuingia kwa ghafl Israel kutoka Ukanda wa Gaza. 

Bendera ya Israel ikiwashwa kwenye jengo la ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza, 10 Downing Street, mjini London kuonyesha uungaji mkono kwa Israel.

Polisi wa Israel wakimuondoa mwanamke na mtoto wake kutoka eneo ambalo roketi iliyofyatuliwa kutoka Ukanda wa Gaza kuanguka katika mji wa Ashkelon, kusini mwa Israel Jumamosi usiku.,

Magari yanawaka moto baada ya roketi iliyofyatuliwa kutoka Gaza kulipuka kwenye eneo la kuegesha magari mjini Ashkelon, kuisni mwa Israel. 

Polisi wa mjini New York wakiwatenganisha waandamanaji wanaoiunga mkono Israel (kushoto) kuwakaribia waandamanaji wanayoiunga mkono Palestina (kulia), kwenye uwanja wa Times Square Oktoba 8, 2023 baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel. 

Moto mkubwa umewaka na moshi umetanda hewani katika mji wa Gaza baada ya jeshi la Israel kudondosha mabomu siku ya Jumapili. 

Wanajeshi wa Israel wakipita katika eneo ambalo halikutajwa karibu na mpaka na Gaza wakati nchi hiyo imetangaza vita na wapiganaji wa Hamas. Oktoba 8, 2023.

Mapigano makali yameripotiwa kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas, siku ya pili baada ya wanamgambo hao kuishambulia Israel. Maandamano ya kuunga mkono pande zote mbili yamefayika katika miji mbali mbali ya dunia.