Wengine kadhaa walijeruhiwa, serikali hiyo iliongeza katika taarifa iliyosomwa kwenye kituo cha televisheni ya taifa, ikibainisha kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Waasi walishambulia boti iliyokuwa imebeba raia katika maeneo yaliyofurika ambayo hutenganisha miji ya Gao na Mopti, wakati wa msimu wa mvua. Boti hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Gao iliposhambuliwa.
Washambuliaji hao pia walivamia kambi ya kijeshi katika eneo la Bourem Circle, lililo katika jimbo la Gao, kaskazini mashariki mwa Mali. Takriban washambuliaji 50 waliuawa katika makabiliano, na siku tatu za maombolezo ya kitaifa zilitangazwa, serikali ya mpito ilisema.
Mali ni mojawapo ya nchi kadhaa za Afrika Magharibi zinazokabiliana na uasi mkali wenye mafungamano na makundi ya al Qaeda na Islamic State, ambao ulikita mizizi kaskazini mwa nchi hiyo, mnamo mwaka 2012.