Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:27

Uingereza kulitangaza kundi la Wagner kama kundi la kigaidi


Bendera yenye nembo ya kundi la Wagner ikipepea kwenye eneo la ukumbusho la muda, kumuenzi marehemu Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa Wagner, Agosti 27, 2023.
Bendera yenye nembo ya kundi la Wagner ikipepea kwenye eneo la ukumbusho la muda, kumuenzi marehemu Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa Wagner, Agosti 27, 2023.

Uingereza Jumatano imesema italitangaza kundi la mamluki la Russia, Wagner kama kundi la kigaidi.

Serikali imesema itawasilisha agizo bungeni na ikiwa litaidhinishwa itakuwa ni kinyume cha sheria kuwa mwanachama au kuliunga mkono kundi hilo.

Agizo hilo litairuhusu pia serikali kukamata mali za kundi la Wagner.

Waziri wa usalama wa ndani Suella Braverman amesema Wagner “imehusika katika uporaji, mateso na mauaji ya kinyama. Operesheni zake nchini Ukraine, Mashariki ya Kati na Afrika ni tishio kwa usalama wa kimataifa.”

Wagner ilihusika katika vita vya Russia nchini Ukraine, na mwezi Juni kiongozi wake Yevgeny Prigozhin alifanya uasi mfupi dhidi ya jeshi la Russia.

Prigozhin aliripotiwa kufariki katika ajali ya ndege mwezi uliopita.

Awali Uingereza iliweka vikwazo kwa Wagner na Prigozhin.

Forum

XS
SM
MD
LG