Mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Doksuri kusini mashariki ya Asia

  • Abdushakur Aboud

Wafanyakazi wa uwokozi watumia boti kupita njia zilizofurika na maji katika mtaa mmoja wa mji mkuu wa China wa Bejing baada ya Kimbunga Doksuri kusababisha uharibifu mkubwa na kuleta mvua nyingi.

Mtu na kijana wake watizama magari yaliyosombwa na maji ya mafuriko katika wilaya ya Mentougou nje ya Bejing.

Bibi harusi atolewa kanisani  mjini Malolos, Ufilipino baada ya mafuriko kutokea mafuriko ndani ya kanisa kufuatia kimbunga Doksuri.
 

 Watu wapita kwenye barabara iliyofurika katika mtaa mmoja mjini Bejing, Uchina, kufuatia kimbunge Doksuri.

Magari yaliyozamani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za siku nyingi kufuatia kimbunga cha Doksuri jijini Bejing.

5Dereva asukuma tuktuk yake katika barabara ya Karachi, Pakistan iliyofurika na maji ya mvua kutonana na mvua za monsoon.

Wakazi wa mtaa mmoja mjini Bejing, China wasubiri kupata majibaada ya mvua nyingi kuharibu huduma za maji.

Watu wanakula na kunywa barabarani katika mji wa Balagtas, jimbo la Bulacan, nchini Ufilipino kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua nyingi zilizosababishwa na kimbunga Doksuri.

Watu 20 wamefariki nchini Uchina na zaidi ya watu 350 000 wamehamishwa kufuatia mafuriko yaliyotokana na moja wapo ya vimbunga vibaya kutokea kusini Mashariki ya Asia.