Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 20:53

Mafuriko yaendelea kusababisha maafa na uharibifu wa mali nchini China


Mapotomoko yaliyosabishwa na mafuriko nchini China
Mapotomoko yaliyosabishwa na mafuriko nchini China

Hali mbaya ya hewa inaendelea kusababisha uharibifu nchini China, ambapo mvua kubwa imesababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko kote nchini.

Katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi, takriban watu wawili waliuawa katika maporomoko ya matope katika viunga vya mji wa Xi'a,n na watu 16 hawajulikani walipo, shirika la habari la serikali lilisema Jumamosi.

Nyumba mbili pia zilisombwa na maji, huku barabara, madaraja na vifaa vya kusambaza umeme pia vikiharibiwa.

Timu za uokoaji zimetumwa kwenye eneo hilo.

Huduma ya treni ilisitishwa Jumamosi mjini Beijing na mji wa kaskazini mashariki wa Harbin, maafisa walisema, kwa sababu ya mvua kubwa na upepo mkali.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa wanajeshi 500 wametumwa katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Jilin, ili kuimarisha uwezo wa kizuizi cha maji, ambacho kudhoofika kwake kunatishia vijiji 29 vilivyo upande wa chini wa mto.

Forum

XS
SM
MD
LG