BUNGE LA UGANDA LIMEPITISHA MSWADA DHIDI YA USHOGA.mp3

Your browser doesn’t support HTML5

Bunge la Uganda limepitisha mswada dhidi ya ushoga kwa mara ya pili, baada ya kurudishwa bungeni na rais Yoweri Museveni akitaka ufanyiwe marekebisho. Kennes Bwire amezungumza na Sadam Mubale, mwandishi wa habari pamoja na mbunge Asuman Baasalirwa, mwandishi wa mswada huo.

Vipengele vitano vimefanyiwa marekebisho ikiwepo kutaka watu watakaopatikana kufanya mapenzi ya jinsia moja kuadhibiwa na wala sio kuwadhibu watu kwa sababu wanashukiwa kufanya ushoga kutokana na wanavyoonekana.
Watakaopatikana na makosa watahukumiwa kati ya miaka 20 gerezani, kifungo cha Maisha au adhabu ya kifo

Mswada huo sasa unasbiri Saini yar ais Yoweri Museveni na kuwa mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya ushoga.