Matukio muhimu ya 2022 katika picha
Mafuriko makubwa kuwahi kutokea Pakistan katika jimbo la Sehwan.
Maji yaliyokauka kwenye ziwa Poyang jimbo la Jiangxi, China ni ishara ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Familia na marafiki wa mwandishi wa habari wa Al Jazeera, Shireen Abu Akleh, aliyeuliwa katika mashambulio ya Israel, wakielekea kumzika.
Olga akimkumbatia rafiki yake Vlodomyr kabla ya kwenda vitani Ukraine, kufuatia uvamizi wa Rashia.
Wakazi walokoseshwa makazi katika kitongoji cha Cite Soleil katika mji mkuu wa Haiti.
Waandamanaji wameingia nyumbani kwa rais Gotabaya Rajapaksa wa Sri Lanka kumtaka aachie madaraka.
Ukame uliokithiri katika jimbo la Abdroy Madagascar, mchanga ukifunika adhi ya mji wa Ambovombe.
Waingereza waaga mwili wa Malkia Elizabeth kuelekea Kasri ya Windsor.
Majengo ya makazi mjini Mariupol yaliyoharibiwa na mashambulizi ya Russia nchini Ukraine
Wakazi wa Obagi, jimbo la River Nigeria wakikimbia mafuriko
Muandamanaji akata nywele zake kupinga sheria ya kuvaa hijab Iran kufuatia kuuliwa kwa Mahsa Amini