Akizungumuza na wanahabari akiwa katika eneo la makaburi ya watu 33 waliouawa kwa mapanga na visu mwaka 2014 Kaskazini Mashariki mwa mji wa Beni wakati wa kuadhimisha miaka minane tangu yaanze mauaji katikatika mwa Mji wa Beni Kivu kasakazini , Rachel Muvunga, mmoja wa wakaazi wa Beni ambao wamepoteza wanafamilia wao, aliomba Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa UN kutangaza rasmi mauaji dhidi ya raia wa Beni, Lubero na hata wa kIturi kuwa ya Kimbari akisema kwamba kila uchao, watu huuawa kwa mapanga na shoka wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Muvunga ambaye amekuwa mwanaharakati kwa zaidi ya miaka thelathini aliomba wananchi pamoja na serikali kushikamana wakati huu mgumu wa mauaji ya kila siku.
Your browser doesn’t support HTML5
Grace Madirisha kwa upande wake anasema mujomba wake aliuawa na waasi wanaodhaniwa kuwa ADF katika Kijiji cha Mkoko siku zilizopita na kuaomba serikali kujenga mnara mjini Beni kama alama ya kihistoria ili mauaji ya Beni yatambulikane kimataifa na kwa vizai vijavyo.
Kundi la vijana wa Lucha nalo limekuwa katika mstari wa mbele kukemea mauaji hayo wakiomba mahakama ya ICC kuendesha uchunguzi dhidi ya watu wanao husika katika mauaji ya Beni, Lubero na Ituri.
Mauaji ya Beni na Lubero yalianza mwaka wa elfu mbili na Kumi katika eneo la Mayi moja na vijiji vingine vinavyopatikana mashambani na watu kadhaa kutekwa na kulazimisha kujiunga na kundi la waasi wa ADF ambao kwa sasa ndio washutumiwa kuhusika natika maachafuko eneo la Beni, Lubero na sehemu moja ya Ituri, serikali ikisema.
-Ripoti imetayarishwa na Austere Malivika, VOA, Goma.