Wanamgambo wa al-Shabaab waliwauwa takribani raia 18 na waliharibu malori yaliyokuwa yamebeba chakula cha msaada katika shambulizi la usiku katika mkoa wa kati nchini Somalia wakaazi na shirika la habari la serikali walisema leo Jumamosi.
Kundi hilo la ki-Islam lilianzisha shambulizi kwenye eneo la Hiran katika jimbo la Hirshabelle lenye serikali yake yenyewe huko kati-kati mwa Somalia. Malori hayo yalikuwa yakisafirisha chakula kutoka jiji la Baladweyne kwenda mji wa Mahas, wakaazi walisema.
Al Shabaab waliwauwa raia 18 na walichoma moto malori kadhaa ya chakula cha msaada yaliyokuwa yakielekea katika mji wa mahas, usiku wa ijumaa, mzee mmoja wa eneo hilo aliliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu.
Wakati huo huo, shirika la habari la Sonna liliripoti kwamba wapiganaji wa al Shabaab walichoma malori yaliyokuwa yamebeba chakula cha msaada kwenda mahas na waliwaua watu wengi waliokuwa kwenye malori hayo.
Kundi hilo la ki-Islam lenye uhusiano na al Qaida limekuwa likipambana na serikali kuu ya Somalia kwa Zaidi ya muongo mmoja. Inataka kuanzisha utawala wake kwa kuzingatia tafsiri kali ya sheria ya ki-Islam.