Mahakama Kuu ya kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi nchini Tanzania, imewakuta Mwenyekiti wa chama cha Upinzani, Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu na kesi ya kujibu kufuatia mashtaka yaliyowakabili ya ugaidi na uhalifu mwingine.
Hayo yamejiri siku mbili baada ya makamu mwenyekiti wa chama hicho na mgombea wa zamani wa urais, Tundu Lissu, kukutana na Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, na kumwambia kwamba angependa kesi hiyo “ifutwe kwa sababu haina msingi wowote.”
Mbowe alikamatwa akiwa mkoani Mwanza alikokwenda kwa ajili ya kuendesha kongamano lililohusu vuguvugu la madai ya katiba mpya.
Baadaye alishtakiwa kwa makosa ya kupanga njama za kutekeleza vitendo vya kigaidi ikiwamo kutaka kuchoma moto vituo vya mafuta na kuwadhuru baadhi ya viongozi wa serikali.
Upande wa mashtaka uliwaleta mahakamani mashahidi 13.
Habari zaidi zitafuata....