Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:28

Ziara ya Rais Xi yatafsiriwa kidiplomasia, mivutano ya Saudia na Marekani yatajwa


Mfalme wa Saudia Arabia Salman na Rais wa China Xi Jinping walipokutana Beijing, China. March 16, 2017. (Lintao Zhang/Pool Photo via AP)
Mfalme wa Saudia Arabia Salman na Rais wa China Xi Jinping walipokutana Beijing, China. March 16, 2017. (Lintao Zhang/Pool Photo via AP)

Rais wa China Xi Jinping atawasili nchini Saudi Arabia siku ya Jumatano kwa  ziara ya siku tatu, ikiwa ya kwanza katika nchi ambayo ni muuzaji mkubwa sana  duniani wa mafuta ghafi tangu mwaka 2016, shirika la habari la serikali ya Saudia limeripoti Jumanne.

Ziara hiyo itajumuisha mkutano wa pande mbili utakaoongozwa na Mfalme wa Saudi Arabia Salman na kuhudhuriwa na Mwana Mfalme Mohammed bin Salman, kiongozi atakayerithi madaraka ya ufalme huo, shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limeripoti.

Xi, kiongozi wa uchumi wa pili mkubwa duniani, pia atahudhuria mkutano wa viongozi kutoka mataifa wanachama sita wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba na mazungumzo yatakayowaleta pamoja viongozi kutoka kwingineko huko Mashariki ya Kati, shirika la habari la serikali lilisema.

Kuwasili kwa kiongozi wa China kumeenda sambamba na kuwepo kwa mivutano ya hali ya juu kati ya Saudi Arabia na Marekani juuya masuala kadhaa kuanzia sera za nishati hadi usalama wa keneo na haki za binadamu.

Pigo la hivi karibuni kwa ushirikiano ambao unakwenda miongo kadhaa nyuma lilitokea Oktoba wakati kundi la wazalishaji mafuta OPEC+ walipokubaliana kupunguza uzalishaji kwa mapipa milioni 2 kwa siku, hatua ambayo White House ilisema ilibainisha “ina mafungamano na Russia” katika vita nchini Ukraine.

Siku ya Jumapili, OPEC+ iliamua kuendelea kupunguza uzalishaji huo.

China ni mteja mkubwa kabisa wa Saudi Arabia wa mafuta ghafi, ikinunua takriban robo ya mafuta ya Saudi Arabia.

Mwana wa Mfalme Mohammed bin Salman alipokutana na Rais wa China Xi JInping walipokutana Beijing China, Feb 22, 2019. (Liu Weibing/Xinhua via AP)
Mwana wa Mfalme Mohammed bin Salman alipokutana na Rais wa China Xi JInping walipokutana Beijing China, Feb 22, 2019. (Liu Weibing/Xinhua via AP)

Zaidi ya nishati, wachambuzi wanasema viongozi hao wa nchi hizo mbili wanatarajiwa kujadili makubaliano muhimu ambayo inaweza kuzipa fursa kampuni za China kushiriki zaidi katika miradi mikubwa ambayo ndiyo kiini cha dira ya Mwana Mfalme Mohammed ya kupanua wigo wa uchumi mbali na mafuta.

Xi mara ya mwisho aliitembelea Saudi Arabia mwaka 2016, mwaka mmoja kabla ya Mwana Mfalme Mohammed kuwa mrithi wa ufalme, katika safari yake iliyomchukua hadi nchini Misri na hasimu wa Saudi Arabia, Iran.

Mwana Mfalme aliitembelea China na kukutana na Xi katika ziara yake ya Asia mwaka 2019.

XS
SM
MD
LG