Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:04

Saudia Arabia kufaidika na Kombe la Dunia


Makumbusho ya Olimpiki na Michezo ya Qatar, Doha, Qatar - Oktoba 10, 2022 Watu wamesimama karibu na jezi za kandanda zinazoonyeshwa.(REUTERS).
Makumbusho ya Olimpiki na Michezo ya Qatar, Doha, Qatar - Oktoba 10, 2022 Watu wamesimama karibu na jezi za kandanda zinazoonyeshwa.(REUTERS).

Saudi Arabia itatoa viza ya kuingia mara kadhaa  kwa mashabiki katika Kombe la Dunia la Qatar, maafisa walisema hivi karibuni huku nchi jirani za Ghuba zikitarajia kufaidika na mashindano hayo.

Saudi Arabia itatoa viza ya kuingia mara kadhaa kwa mashabiki katika Kombe la Dunia la Qatar, maafisa walisema hivi karibuni huku nchi jirani za Ghuba zikitarajia kufaidika na mashindano hayo.

Watu wenye kadi iitwayo Hayya, ambayo imetengwa kwa wale wenye tiketi na kutumiwa kuingia Qatar wakati wa mashindano, wataweza kutuma maombi ya visa kwa njia ya kielektroniki, wizara ya mambo ya nje ilisema.

Hatua hiyo imekuja wakati Qatar, ambayo ina wakazi milioni 2.8, inajaribu kuhudumia wageni milioni 1.2 wanaotarajiwa wakati wa Kombe la Dunia litakalofanyika Novemba 20 hadi Desemba 18, na huku Saudi Arabia ikiongeza juhudi za kuvutia watalii.

Watu walio na kadi iitwayo Hayya, ambayo inatolewa kwa wenye tikiti na kutumika kuingia Qatar wakati wa mashindano, wataweza kutuma maombi ya visa vya kielektroniki, wizara ya mambo ya nje ilisema.

Wale wenye visa wataweza kuingia na kutoka katika Ufalme huo mara kadhaa wakati visa yao muda wakutumika haujakwisha, wizara hiyo ilisema kwenye Twitter.

Visa za Saudia zitaanza kutumika siku 10 kabla ya kuanza Kombe la Dunia na itatumika kwa siku 60.

Kwa kuzingatia shinikizo la malazi nchini Qatar, Saudia, Kuwait Airways, flydubai na Oman Air zitaweka zaidi ya safari 160 kila siku za ndege ili kuwapeleka mashabiki kwenye safari za kila siku mchana kwa ajili ya mechi.

Maafisa wa Qatar wanasema zaidi ya mashabiki 20,000 wanaweza kuwasili kila siku kwa ndege kutoka nchi za Ghuba, ambazo baadhi zinatoa ofa maalum za hoteli.

Idadi kubwa ya Wasaudi pia watafurika kuvuka mpaka. Mechi ya Saudi Arabia ya Kundi C dhidi ya Argentina ya Lionel Messi ni moja ya michezo inayongojewa sana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kombe la Dunia Nasser al-Khater aliliambia Shirika la Habari la Qatar katika mahojiano ya Twitter hivi karibuni.

Hatua hiyo ya viza imekuja licha ya Saudi Arabia, Bahrain, UAE na Misri kukata uhusiano na Doha mwezi Juni 2017, zikiituhumu kuwa karibu na Iran na kuunga mkono makundi yenye itikadi kali, tuhuma ambazo Qatar ilikanusha. Vizuizi vya kidiplomasia, biashara na usafiri viliondolewa Januari 2021.

XS
SM
MD
LG