Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:24

Zelenskiy atembelea kiwanda cha kutengeneza silaha katika jimbo la Pennsylvania


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy

Chini ya ulinzi mkali, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Jumapili alikitembelea kiwanda cha kutengeneza silaha katika jimbo la Pennsylvania.

Ziara yake kwenye kiwanda cha zana za kijeshi cha Scranton inajiri wakati wiki hii Marekani imeandaa shughuli nyingi kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Russia.

Zelenskiy atazungumza katika mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wa kila mwaka jijini New York Jumanne na Jumatano, na kisha atafanya ziara Washington kwa ajili ya mazungumzo na Rais Joe Biden na Makamu wake Kamala Harris Alhamisi.

Wakati msafara mkubwa wa magari wa Zelenskiy ulikuwa ukielekea kwenye kiwanda hicho Jumapili, kundi dogo la wafuasi wake walipeperusha bendera za Ukraine wakikusanyika karibu ili kuonyesha shukrani zao kutokana na ziara yake ya kuwashukuru wafanyakazi.

Kiwanda hicho cha Scranton ni moja ya viwanda vichache vinavyotengeneza makombora ya mizinga na kiliongeza uzalishaji wa makombora hayo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Forum

XS
SM
MD
LG