Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 02:25

Zambia yapitisha sheria mpya ya Upatikanaji wa Taarifa


Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa Ufaransa. Picha na Geoffroy VAN DER HASSELT / AFP.
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa Ufaransa. Picha na Geoffroy VAN DER HASSELT / AFP.

Zambia imekuwa nchi ya hivi karibuni kupitisha sheria ya Upatikanaji wa taarifa, wakati Rais Hakainde Hichilema aliposaini mswaada mwezi uliopita, zaidi ya miaka 20 tangu mswaada huo ulipowasilishwa bungeni.

Wakati baadhi ya watu wakifurahia hatua hiyo, wanaharakati wa haki wanasema sheria hiyo haijafikia viwango vya kimataifa.

Chini ya Sheria mpya, kila raia anaweza kuomba taarifa ambazo si za siri kutoka serikalini kuhusiana na suala lololote lenye kwa maslahi ya umma.

Msemaji wa Muungano wa Mashirika ya Kiraia ya Zambia au ATI Grant Tungay, amesema sheria mpya haijakamilika, lakini ni mwanzo mzuri.

Sheria mpya ina lengo la kutoa haki ya upatikanaji wa taarifa kama inavyotakiwa na mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya rushwa na mkataba wa Afrika kuhusu haki za binadamu na watu.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, upatikanaji wa taarifa unahamasisha ushiriki wa raia katika utawala, kuwafanya raia waiamini serikali zaidi na kuongeza uhalali wa taasisi za umma

Forum

XS
SM
MD
LG